Men The Podcast

Ep 41 - Finding your purpose

Aug. 26, 2021

Kwa nini unaishi? Ni kipi ambacho unakitaka maishani? Ni kipi unachokithamini? Upo tayari kukifanyia kazi ili kukipata? Upo tayari kuachana na yale ambayo yanasimama katikati ya wewe na kufikia pale unapotaka kufika? Upo tayari kulipa gharama za kuweza kufika pale? Na zaidi ya yote, KWA NINI hicho kitu ni muhimu kwako? Safari ya miasha inakuja na mambo mengi sana, méngine tunaweza yaelezea mengine hatuwezi ila ukweli ni kwamba watu wengi sana bado tupo kwenye safari ya kujitafuta na ya kuweza kuelewa kwanini tupo hapa duniani. Ben Owden ameweza kuwa wazi na kuelezea safari aliyopitia yeye ili aweze kujitambua. Ameeleza mafanikio na changamoto za safari hii yenye milima na mabonde, jasho na machozi na mchakato mzima (process) muhimu kwa mtu kupitia ili aweze kuwa mtu bora zaidi

Podparadise.com neither hosts nor alters podcast files. All content © its respective owners.